Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe (65), anatarajia kutangaza nia yake ya kujiuzulu leo Ijumaa Agosti 28, kutokana na matatizo ya kiafya

Taarifa kutoka kituo cha televisheni ya serikali NHK, zinasema Waziri mkuu, ambaye amepatwa na ugonjwa wa matumbo sugu, ameelezea nia yake ya kujiuzulu ili kuepuka kuvuruga hali ya kisiasa ya kitaifa

Mwaka 2007 aliwahi kujiuzulu nafasi ya Waziri mkuu kutokana na tatizo hilihili linaloathiri utumbo mkubwa ambalo amekuwa akiishi nalo tangu akiwa kijana

Abe amekuwa Waziri mkuu wa Japan tangu mwaka 2012, na anatajwa kuwa Waziri mkuu aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi kirefu zaidi Japan

Viongozi wawasili Ukerewe kudhibiti mauaji
Kalemani: Ufaransa, Norway mmetuwezesha kutekeleza miradi ya umeme