SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa kongamano la siku mbili la uwekezaji litakalojadili mipango madhubuti ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 -22 Julai mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamis Issa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo.

Dkt. Issa alisema Serikali imepitisha Sera ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya Mafuta na Gesi asilia, hatua ambayo itasadia wananchi wazawa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

“Msukumo mkubwa wa serikali kwa sasa ni kuongeza ushiriki katika  uwekezaji unaochochewa na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kina kirefu cha bahari  ambao utaweza  kuwanufasha Watanzania” alisema Dkt. Issa.

UEFA Yataja Wanaowania Tuzo Msimu Wa 2015-16
Mashirika Ya Kidini Kuimalisha Mahusiano na Serikali Katika Utendaji Kazi