Baada ya siku 10 za maombolezo ya Malkia Elizabeth II, Waingereza wamerejea katika maisha ya kawaida ili kukabiliana na hali halisi ya maisha ya kila siku, huku Waziri mkuu mpya, Liz Truss, akihudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York na Serikali yake inatarajia kutoa mipango mikubwa ya kukabiliana na shida za kiuchumi na kijamii.

Akiwa njiani kuelekea New York, Truss amesema Uingereza haikutarajia makubaliano ya kibiashara ya Marekani katika “muda mfupi hadi wa kati” na kukiri kuwa baadhi ya wachambuzi walisema ilikuwa na lengo la kuondoa nguvu ya utawala wa Biden katika kuishinikiza Uingereza kusuluhisha mzozo na Umoja wa Ulaya.

Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Liz Truss. Picha na NPR

Katibu mpya wa afya wa Uingereza, Thérèse Coffey na Kansela mpya wa Hazina, Kwasi Kwarteng pia wanatarajia kuelezea mipango yao ya kukabiliana na shinikizo linaloongezeka kwa huduma za afya na uchumi ambapo Kwarteng lazima aeleze jinsi anavyoweza kufadhili ahadi zake za kuwakinga wateja na biashara kutokana na kupanda kwa gharama za nishati baada ya kupunguza ushuru.

Miongoni mwa mipango ya serikali yanayotarajiwa kuwepo katika ajenda ni pamoja na kumalizika kwa kikomo cha bonasi kwa mabenki na kusitishwa kwa uvujaji wa fedha za Serikali huku wote wawili wakiwa na matumaini chanya katika mikakati yao muhimu ya kufanikisha mipango waliyojiwekea.

Waandamana kupinga mauaji, sheria ya Hijab
Hatua za Rais Samia nchini Msumbiji