Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi watendaji wateule 185 wa majiji, manispaa, miji na halmashauri za wilaya waende wakafanye kazi kwenye maeneo yao mapya waliyopangiwa kwa kuzingatia uadilifu, uwajibikaji na uaminifu.

Wito huo umetolewa na Waziri Mkuu leo wakati akizungumza na wateule hao kabla hawajatoa viapo ya maadili katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Jukumu mlilopewa na Mheshimiwa Rais ni nyeti na linahitaji utulivu na kujituma. Kila mmoja wenu anatakiwa akafanye kazi kwa uadilifu, uwajibikaji na uaminifu,” – Waziri Mkuu

“Ninyi ndiyo injini ya maendeleo katika Halmashauri zote hapa nchini na pia mna dhamana ya kusimamia fedha za maendeleo katika halmashauri zenu. Mtajikuta mna jukumu la kusimamia fedha za ndani pamoja na fedha zinazotoka Serikali Kuu. Hakikisheni mnasimamia matumizi ya fedha hizi ili kupata value for money.” Waziri Mkuu

Pia Majaliwa aliwataka wawe makini wasije wakajikuta wanaingia kwenye migogoro ya kifedha dhidi ya watendaji wengine, migogoro ya kikazi na pia migogoro na wananchi wanaoenda kuwaongoza.

Amewasihi Wakurugezi hao kushirikiana na wadau wengine ambao ni wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, kamati za ulinzi na usalama, wakuu wa idara, watumishi wa idara mbalimbali zilizo chini yenu na watendaji wa kata na vijiji.

Alisema wanatakiwa wakasome taarifa mbalimbali ili waelewe majukumu yao pamoja na mipaka yao, waelewe maeneo yao ya utawala ni yapi lakini pia wajipange kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwani imebeba ahadi zilizotolewa na Rais pamoja na Makamu wa Rais wakati wa kampeni za uchaguzi.

Aliwaasa pia wasiache kutafuta hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuzindua Bunge la 11, aliyoitoa Novemba 20, mwaka jana na kuwataka waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha kwa vile inatoa dira ya utendaji katika maeneo yao.

Q Chief Afungukia Mchango wa Diamond kwenye Muziki
Rais Museven Azua Mjadala Mtandaoni