Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaonya wafanyabiashara watakaojaribu kupandisha bei za vyakula wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza leo katika shughuli ya maombi maalum ya kuliombea Taifa dhidi maambukizi ya virusi vya corona, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanafuatilia mwenendo wa bei sokoni.

“Ninatoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kutembelea masoko mara kwa mara kuona hakuna sababu ya kupandisha huduma zinazotolewa kwenye masoko yetu, eti kwa sababu baadhi ya Watanzania wanaingia kwenye Mwezi Mtukufu,” amesema Waziri Mkuu na kuongeza kuwa kwa kupandisha bei hawezi kupata baraka.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa kuna sukari ya kutosha nchini hivyo bei itaendelea kuwa ileile bila kujali msimu.

Amewaagiza wakuu wa Mikoa kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara watakaouza sukari kwa bei ya kuanzia Shilingi 4,500.

Wakenya kupewa fedha za ruzuku ya athari za corona

Rwanda yatengeneza mashine ya kupumulia wagonjwa wa Covid 19

Papa Francis atoa wito Umoja wa Ulaya
Rwanda yatengeneza mashine ya kupumulia wagonjwa wa Covid 19