Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa  juu ya ualbino yatakayofanyika Juni 13 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania, Nemes Colman Temba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuibua mijadala na tafakuri kwa wadau juu ya ukusanyaji endelevu wa takwimu, uchambuzi na upatikanaji wa watu wenye ualbino kwa wakati ili Serikali iweze kuwasajili,  kuwahudumia na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanakuwa salama.

“Bila ya utaratibu mzuri wa upatikanaji wa Takwimu Serikali haitaweza kupanga vyema juu ya ustawi wa watu wenye ualbino, hivyo maadhimisho ya mwaka huu yataibua mjadala wa umuhimu wa upatikanaji wa takwimu sahihi kutoka ofisi ya Taifa ya takwimu kwaajili ya kusaidia katika mipango ya maendeleo ya watu wenye ualbino”,amesema Temba.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyojumuisha takwimu za watu wenye ualbino ilisaidia kubaini idadi ya watu hao ambapo walikuwa 16,376 wakiwemo Wanaume 7,620 na Wanawake 8,756.

 

Zitto ataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya askari polisi aliyemtishia bunduki Malima
LEMA awashangaa wanaomdhihaki baada ya kumpongeza Nyalandu