Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amesema Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’, ambao unafanyika leo Jumatano (Agosti 10) jijini Arusha utafungua fursa kwa Tanzania ya kuandaa mashindano makubwa.

Akifungua mkutano huo ambao unafanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa ya Arusha ‘AICC’ Waziri Mkuu alisema anaamini mkutano huo utafungua njia kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mikutano mingine ya CAF pamoja na FIFA.

Alisema Tanzania kupitia ‘TFF’ imekuwa na mahusiano mazuri na ‘CAF’ pamoja na ‘FIFA’ na imekuwa ni chachu ya kuhamasisha na kuimarisha maendeleo ya Soka nchini na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Motsepe: Afrika inapaswa kupiga hatua kwa kazi kubwa

“Ujenzi wa vituo viwili vya michezo nchini chini ya ‘TFF’ kwenye miji ya Tanga na Dar es Salaam ni kielelezo cha mahusiano mazuri na tunaishukuru sana ‘FIFA’ kwa uwekezaji huo”. amesema Majaliwa.

Aliongeza kuwa ni matarajio ya Tanzania kuwa ‘FIFA’ itaendelea kubuni miradi mingi ya kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya ujenzi wa miundombinu ya mchezo.

Majaliwa alisema Tanzania kwa upande wake iko tayari kuendelea kuimarisha uhusiano wake na ‘FIFA’ na wanachama wake ‘CAF’.

“Mashindano ya mpira wa miguu kwa Shule yani African Schools Football Programe mliyoanzisha ni njia sahii ya uwekezaji wa muda mrefu na maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika”. alisema Majaliwa.

Kocha Singida Big Stars aipa mtihani Young Africans
Motsepe: Afrika inapaswa kupiga hatua kwa kazi kubwa