Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Ariel Henry  ameahidi kufanyika uchaguzi wa haraka wa Taifa hilo, kufuatia kuuwawa kwa aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Jovenel Moise huku bado kukiwa na vurugu za maandamano ya wananchi ya kupinga Mataifa ya kigeni kuingilia siasa za ndani.

Amesema mpango wa serikali yake ni kufanikisha uchaguzi huru, wa kuaminika, wenye uwazi ambao utawashirikisha wapiga kura wengi.

“Majadiliano hadi wakati huu bado magumu lakini yenye tija. Mazungumzo yanatoa umuhimu wa maridhiano kwa taifa la Haiti.” amesema Henry.

Waziri mkuu huyo amesisitizaumoja na kuongeza kwamba angependa muundo mpya wa Serikali, ambao utakuwa na uwazi pamoja na yote usizongwe na rushwa.

Mkutano huo ambao umedumu kwa takribani dakika 10, umefanyika katika kipindi cha tofauti ya masaa machache baada ya Henry kukutana na baraza la Mawaziri katika mkutano wa ndani.

Katika mkutano huo, inataarifiwa  kwamba alitoa taarifa ya maendeleo ya uchunguzi wa mauwaji ya Julai, 7  ya Rais Moise ambaye  aliuwawa akiwa katika makazi yake binafsi kwenye mkasa ambao pia mke wake alijeruhiwa vibaya.

Burundi yaridhia kupokea chanjo ya Uviko 19
Watoa huduma za mawasiliano watakiwa kuzingatia sheria, kanuni