Wazir Mkuu wa Israel Naftali Bennett ameachia madaraka ya nafasi hiyo ambapo serikali ya nchi hiyo imemtangaza Yair Lapid kama Waziri Mkuu mpya nchi hiyo.

Lapid ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Centrist ataliongoza Taifa hilo hadi kufikia Uchaguzi Mkuu wa Novemba 1.

Lapid anajiandaa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu alipania kurudi tena madarakani.

Naftali Bennett alikabidhi madaraka kwa Lapid kama yalivyo makubaliano ya kubadilishana madaraka ya Uwaziri Mkuu, ingawa Bennett amebainisha kuwa hatagombea tena uchaguzi wa mwezi Novemba.

Waziri wa zamani wa nchi hiyo na Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu Benjamin Netanyahu amepongeza hatua hiyo akidai kuwa ni hatua muhimu sana kwa maendeleo ya siasa na demokrasia ya Taifa la Israel.

Mangungu: Kocha Zoran atashiriki usajili 100%
Muhimbili inafanya upasuaji watoto walioungana