Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson (55) amelazwa hospitalini ili kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu zaidi kutokana na kuendelea kuonesha dalili za virusi vya corona ikiwa ni siku 10 tangu athibitike kupata maambukizi.

Taarifa iliyotoka kwenye ofisi yake, Kiongozi huyo bado anaonesha dalili za virusi vya covid19 siku 10 baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo mnamo Machi 26.

Aidha waziri wa nyumba wa Uingereza Robert Jenrick amesema ni matarajio yao kwamba kutokana na vipimo alivyofanyiwa atarudi na kuendelea na majukumu yake hivi karibuni.

Jenrick amesema waziri mkuu huyo ataendelea na majukumu yake ya kuliongoza taifa la Uingereza hata akiwa hospitalini

Hata hivyo ofisi yake imebainisha kwamba kulazwa kwake hospitalini si jambo la dharura bali ni kutokana na ushauri wa daktari wake kama njia ya tahadhari

Johnson aliwekwa karantini katika makazi yake yaliyopo Downing St. tangu kupatikana na corona  mnamo Machi 26

Hadi, kufikia Jumapili, takriban watu 48,000 walithibitishwa kuwa na corona  Uingereza na takribani watu 4,934 wakipoteza maisha

Yanga yapewa ushauri wa bure
Gonzalez ajinyonga baada ya kukutwa na Corona