Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ametangaza uamuzi wa kujiuzulu katika nafasi hiyo mwezi Oktoba mwaka huu kupisha utawala mpya.

Umauzi huo wa Cameron umekuja muda mfupi baada ya raia wengi wa Uingereza kupiga kura kutaka kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya (EU). Jitihada za Waziri Mkuu huyo kuwashawishi wananchi wake wasikubali kujiondoa kwenye umoja huo kutokana athari za kiusalama na kiuchumi zitakazowakabili ziligonga mwamba.

Matokeo ya kura za maoni yaliyotangazwa leo yameonesha kuwa asilimia 52 ya wananchi wametaka kujiondoa EU huku asilimia 48 ikitaka wasijiondoe.

Matokeo ya EU

Cameron ametangaza uamuzi huo wa kujiuzulu akieleza kuwa atajitahidi sana ‘kuvuta kamba’ katika nafasi hiyo kwa wiki chache zijazo lakini uongozi mpya unahitajika.

Wakazi wengi zaidi wa jiji la London na Scotland ndio waliopiga kura nyingi zaidi kutaka waendelee kubaki EU walikodumu kwa miaka 43 hadi sasa, lakini wananchi wamaeneo mengine waliwazidi.

Video Mpya: Godzilla - Nataka Mkwanja
Sterling Pound Yaporomoka, Ipi Hatima ya Uingereza!