Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amerudi rasmi kazini baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa katika Hospitali ya Bejamin Mkapa Mkoani Dodoma.

Februari 23,2021 aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo ambapo kabla hajaondoka Hospitali alizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa anaendelea vizuri huku akibainisha tofauti ya hali yake kiafya wakati anapelekwa hospitalini hapo na siku hiyo.

“Afya yangu imeimarika vizuri kabisa kabisa, Jopo letu la Madaktari wameona nina afya njema, nina uwezo wa kuanza kurudi kuendelea na shughuli za kulitumikia Taifa letu, narudi kazini, kazi ndogondogo nimeshaanza, niwaombe Watanzania tuendelee kumuomba Mungu atatuvusha, amenivusha mimi naamini wagonjwa wenzangu watapona,” alisema Mpango.

“Nimeona niseme haya ili mjue naendelea vizuri na nimerudi kazini kwahiyo mjue kibarua wenu wa kwenda kusimamia mapato na matumizi ya Serikali, utafutaji wa mikopo na misaada na kulinda nidhamu ya matumizi ya Serikali amerudi kazini,” aliongea Waziri Mpango.

Kitufe kifuatacho kinakupeleka kutazama video inayomuonesha Ofisini kwake baada ya kurejea.

Kalemani awapa TANESCO siku tano
Mfahamu Othman Masoud, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mrithi wa Maalim Seif