Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa rai yake kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Soka nchini TFF kumtimua kocha Emmanuel Amunike

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa kama TFF wameamua kufuata nyayo za Misri katika kumfuta kazi Amunike basi na wao wanapaswa wakamilishe mchakato kwa kujiuzulu nafasi zao.

”Sisi hatuna tatizo na maamuzi ya TFF endapo tu yatatupeleka mbele, lakini kama ni uamuzi wa kuwaiga Wamisri baada ya kutolewa AFCON, hayo ni makosa makubwa sana kwa sababu kama unaiga basi nao wakamilishe kwa kujiuzulu safu nzima ya uongozi”, amesema Waziri Mwakyembe.

Aidha, amesema kuwa ubabaishaji katika soka hawezi kukubaliana nao ambapo amesema ni bora kuishia kucheza karata kuliko kuingia kwenye soka la ubabaishaji na kuingia kwenye mipango ya hovyohovyo na wanaoharibu hakuna anayewajibika.

Pia amesema kuwa hadi kufikia 24 Julai mwaka huu, benchi la ufundi la Taifa Stars na Viongozi wa TFF wanatakiwa kutoa ripoti yao ya michuano ya AFCON kwa ajili ya kujadiliwa.

Hizi hapa nafasi za kazi kutoka makampuni 10, ‘Apply hapa’
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 11, 2019