Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mtangazaji Mahiri wa Clouds Media Group, Ephraim Samson Kibonde kilichotokea jana Jijini Mwanza.

“Msiba huu ni pigo kubwa kwetu wanatasnia wa habari nchini, tupo pamoja na wenzetu wa Clouds Media Group katika kipindi hiki kigumu cha majonzi” amesema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, enzi za uhai wake Marehemu Kibonde alikuwa Mtangazaji wa Redio ya Clouds FM katika kipindi cha Jahazi, pia alijihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo uandaaji wa  vipindi vya kuelimisha Umma katika masuala ya Makazi na Afya.

Hata hivyo, Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, uongozi na wafanyakazi wote wa Clouds Media Group pamoja na wadau wa habari nchini.

Makala: Wafahamu wanawake wa chuma walioibadili dunia kuwa ilivyo leo
Rais Kagame amaliza ziara yake hapa nchini