Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wiki hii alitembelea ofisi ya WCB iliyopo Tandale jijini Dar es salaam na kujionea uwekezaji uliofanywa na label hiyo ambayo ipo chini ya Diamond Platnumz.
Mh. Waziri wa wizara mambo ya ndani, Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea ofisi za WCB na kukutana na baadhi ya wafanyakazi na wasanii wa label hiyo ili kuwapa moyo na kuwahakikishia kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakikisha kazi zao zinalindwa kwa mujibu wa sheria. Kwani mchango wao katika kuibadilisha tasnia ya muziki wa Tanzania kuwa fursa ya kibiashara na kazi rasmi umeonekana kwa asilimia kubwa.

Pia kawajulisha kuwa serikali haitasita kuwapa msaada pale watakapokwama na kuhitaji usaidizi wa serikali.

”Binafsi nimeona ni jambo jema hasa ukizingitia wameshatembelea viongozi na mawaziri kadhaa. Rai yangu kwa wasanii wengine kuiga mfano wa WCB katika kuwa na ofisi maalumu na kuzipa thamani kazi zao”. Alisema Waziri.
 Baada ya kumaliza mazungumza hayo, Waziri Nchemba kupitia instagram yake aliandika:#Wizi wa kazi za wasanii #Jeshi la polisi kuongeza nguvu

Ubabe wa Faru John na kuwapanda wanae vyatajwa kumgharimu, Maghembe anena
Waliokamatwa malawi sio majasusi