Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba, amekemea vikali wananchi wanaotaka kuijaribu serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli, kwa kupora haki za watu hivyo ameeleza kuwa lazima watu hao waonyeshwe kwamba serikali haijaribiwi na haki za wananchi haziwezi kuchezewa.

Ametoa angalizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Shinyanga.

Msihangaike na jambo limetokea wapi badala yake uhalisia utumike kufanikisha utoaji wa maamuzi, ndugu zangu Rais wetu ana maono ya kutetea haki hivyo sisi  wasaidizi wake tunapaswa kuhakikisha kuwa wananchi wanatendewa haki pasina kuonewa“, amesema Waziri Nchemba.

Katika kikao kazi hicho Nchemba, amemuagiza mkuu wa wilaya ya Kahama, kuandaa na kusimamia utaratibu wa kisheria kuhakikisha kuwa hakuna jambo lolote litakalofanyika ikiwemo mauziano bubu ya mali za mlalamikaji huyo hadi pale shauri lililoko mahakamani litakapokamilika.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 17, 2020
Uganda: Tume ya mawasiliano yaitaka google kufunga vituo hivi Youtube