Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema ni muhimu uwekezaji uwekewe kipaumbele katika sekta za uzalishaji zikiwemo za mifugo na uvuvi ili nchi iweze kuuza maziwa nje ya nchi.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji kazi wa Bodi ya Maziwa nchini kwa kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Uvuvi amesema matatizo mengi yanaweza kutatuliwa katika tasnia ya maziwa na uzalishaji wa tasnia hiyo ili kukuza wigo wa upatikanji wa kutosha wa maziwa katika ngazi ya uzalishaji.

“Suala hili la uwekezaji linapokuwa dogo linatuathiri katika maeneo mengi, kwa kweli unahitajika uwekezaji wa kutosha katika tasnia ya maziwa ili kuongeza uzalishaji na kuweza kuuza maziwa nje ya nchi.” Amesema Waziri ndaki

Aidha amesema serikali imekuwa ikihimiza wafugaji kuwa katika vyama vya ushirika kama nyenzo ya kuweza kuwafikia wafugaji kwa uhakika ili kuzalisha na kukusanya maziwa katika mfumo rasmi kwa ajili ya kutumika katika viwanda vya kuchakata maziwa nchini.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini Dkt. George Msalya amesema asilimia 80 ya maziwa yanayozalishwa hapa nchini hayapo katika mfumo rasmi hivyo inahitajika jitihada zaidi ili yawe kwenye mfumo huo kwa ajili ya kujulikana ubora wake kabla ya kutumika kwenye viwanda vya kuchakata maziwa nchini.

Amefafanua kuwa bado tasnia ya maziwa katika mchango wa taifa ni mdogo licha ya kwamba bodi imekuwa ikiendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha unywaji wa maziwa unaongezeka nchini.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji Dkt. Christine Ishengoma amesema ni muhimu kwa wafugaji kwa sasa kubadili fikra zao na kufuga kisasa kwa kuwa na ng’ombe wachache wenye uwezo wa kutoa maziwa mengi.

Amebainisha kuwa ni vyema kuwepo na mikakati ikiwemo ya takwimu ili kufahamu kiasi sahihi cha maziwa kinachozalishwa nchini kutoka kwa ng’ombe wa asili na walioboreshwa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (Mb), akifafanua jambo na kujibu maswali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji kazi wa Bodi ya Maziwa nchini jijini Dodoma, ambapo Mhe. Ndaki amesema ni muhimu uwekezaji uwekewe kipaumbele katika sekta za uzalishaji zikiwemo za mifugo na uvuvi ili nchi iweze kuuza maziwa nje ya nchi.
Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini Dkt. George Msalya akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa bodi hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma na kufafanua kuwa asilimia 80 ya maziwa yanayozalishwa hapa nchini hayapo katika mfumo rasmi hivyo inahitajika jitihada zaidi ili yawe kwenye mfumo huo kwa ajili ya kujulikana ubora wake kabla ya kutumika kwenye viwanda vya kuchakata maziwa nchini
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akifafanua jambo wakati wa kuhitimisha kikao kilichopokea taarifa ya utendaji kazi wa Bodi ya Maziwa nchini jijini Dodoma, na kusema kuwa ni muhimu kwa wafugaji kwa sasa kubadili fikra zao na kufuga kisasa kwa kuwa na ng’ombe wachache wenye uwezo wa kutoa maziwa mengi
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Kulia) akiwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Amosy Zephania wakati wakisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa wajumbe (hawapo pichani) wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji kazi wa Bodi ya Maziwa jijini Dodoma

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 22, 2021
Mfumo wa utoaji vyeti vya Uviko 19 kwanjia ya mtandao wapata hitilafu