Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amempa siku saba Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, ahakikishe wastaafu wote wa jeshi la polisi wanaodai mafao yao wanalipwa.

Ametoa maagizo hayo leo Februari 26, 2021, wakati akizungumza na Askari Polisi pamoja na wananchi mara baada ya kuzindua Chuo cha Maafisa wa Polisi Kurasini Dar es Salaam.

Ambapo awali IGP Sirro alimuomba Rais Magufuli awasaidie wastaafu ambao hawajalipwa mafao yao waweze kulipwa kwa wakati.

“Waziri Simbachawene nakuagiza nenda kashughulikie malipo ya wastaafu na ikiwezekana ndani ya wiki moja wawe wamelipwa, tuliwatumia vizuri wakati hawajastaafu ni lazima wafaidike na kustaafu kwao hakuna kinachoshindikana pesa ipo,” amesema Rais Dkt. Magufuli.

JPM aiagiza TAKUKURU kuichunguza Manispaa ya Temeke
Kim Poulsen ataja jeshi la Taifa Stars