Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa msemaji wake, Haji Manara imemtangaza Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry utakaochezwa Jumatano Machi 7.

Taarifa ya Manara imeeleza kuwa Waziri Tizeba ndiye ataongoza maelfu ya mashabiki wa soka nchini watakaojitokeza kwenye uwanja wa taifa kushuhudia mtanange huo.

”Waziri wa kilimo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Charles Tizeba anatarajiwa kuongoza maelfu ya wanasimba na watanzania kuishangilia Simba kwenye mchezo huo,”imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, Mchezo huo wa hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Afrika kusini.

Wakati Simba ikisubiri mchezo wake wa Jumatano wapinzani wao Yanga watakuwa dimbani kesho jioni kuumana na wageni wao Township Rollers ya Botswana kwenye uwanja wa taifa.

 

Video: Serikali kulipa madeni ya watumishi wa umma
Msafara wa Polepole wapata ajali