Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na watoto, Ummy Mwalimu amezitaka hospitali zote za rufaa za Wilaya nchini kuwa na Wodi ya wazazi ili kuepusha vifo vya wazazi na watoto wachanga.
Waziri Ummy amesema baada ya miezi sita zinatakiwa zikamilike vinginevyo atazishusha hadhi Hospitali za Wilaya ambazo hazitokuwa na Wodi za wazazi.
Waziri Ummy amesema hayo leo Februari 13, 2017 katika hospitali ya rufaa ya Temeke, katika makabidhiano ya vifaa tiba vya Afya ya uzazi ambavyo vimetolewa na CCBRT kwa ajili ya kusaidia wazazi na watoto, vifaa tiba hivyo vinagharama ya milioni 200.
Pia, Waziri Ummy ameishukuru CCBRT kwa mpango mkakati huo unaoenda sambamba na wizara na taifa kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto za afya ya uzazi mkoani Dar es salaam.
Amesema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana kwani imepelekea kupungua kwa 30% ya vifo vitokanavyo na uzazi katika mkoa wa Dar es salaam kutokana na kupatikana kwa vifaa tiba.
Moja ya changamoto iliyoonekana wakati wa ziara hiyo fupi katika hospitali ya Temeke ni upungufu wa wa wafanyakazi pamoja na majengo huku wakisisitiza kuongezewa vifaa tiba kwa ajiri ya kuboresha huduma zao.

Vigogo watema 'cheche' kuhusu dawa za kulevya
Video: Kamishna madawa ya kulevya aanza makali