Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka viongozi wa Mkoa wa Rukwa kusimamia fedha za dawa pamoja na upatikanaji wa dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vilivyopo kwenye mkoa huo.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akiongea na viongozi na watumishi wa Wilaya na mkoa wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani hapa.
“Nahitaji mfamasia awe anaprinti karatasi yenye kuonyesha dawa zilizopo kwenye stoo yake ili mganga anayeingia zamu siku hiyo aweze kujua dawa zilizopo na kumuandikiamgonjwa wake kuliko kuanmdika dawa ambazo hazipo kituoni hapo
Pia, amewapongeza mkoa huo kutokana na kuwa na hali nzuri nya uwepo wa dawa katika vituo vyote alivyotembelea ingawaje bado kuna changamoto ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu uchangiaji wa dawa na kuwataka wakimaliza dawa walizonazo stoo zikiisha wanatakiwa kupunguza bei za dawa ili wananchi waweze kupata dawa hizo pasina shaka
“Rais amesema hataki kuona wananchi wanapata shida ya upatikana wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali hivyo akaongeza bajeti ya dawa kwa miaka miwili mfululizao”akitolea mfano kwa mkoa wa Rukwa ,mwaka 2016/2017 bajeti ya dawa iliongezeka kutoka milioni 495 hadi kufikia bilioni 1.4 na kwa mwaka huu 2017/2018 imeongezwa na kufikia bilioni 2.02.
Amesema upatikanaji wa dawa huo utaongezeka kutokana na kwamba hivi sasa serikali kupitia bohari ya dawa(MSD) inanunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wa ndani tofauti na zamani ambapo walikua wakinunua toka kwa mawakala
Pamoja na changamoto zote zinazowakabili katika vituo vya kutolea huduma, Waziri Ummy ameupongeza mkoa huo kwani bado unasonga mbele katika kukabiliana na tatizo la vifo vitokanavyo na na uzazi kwa vifo 117 kati ya vizazi hai laki moja wakati takwimu za kitaifa ni vifo 506

Dkt. Shein aeleza anayefanya maamuzi ya CCM, akagua mradi wa visima
Picha: Simba waanza mkutano wa mabadiliko