Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu amesema Serikali imejiwekea mikakati katika Sekta ya Elimu kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa walimu wanaofanyakazi katika maeneo magumu na mbali kufikika na kupata maeneo ya kuishi.

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara katika shule ya Sekondari ya Ugala River iliyopo katika kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu, akiwa ameambatana na Viongozi wa Mkoa na Wilaya wakati akikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Ugala River, iliyopo katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi
Madarasa yanayojengwa katika shule ya Sekondari ya Ugala River katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi lengo ni kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule hiyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja viongozi wa Mkoa na Wilaya kwenye nyumba ambayo wanaishi waalimu wa shule ya sekondari Ugala River, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Kigoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu akiwa ameambatana na Viongozi wa Mkoa na Wilaya wakati akikagua ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Ugala River, iliyopo katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu akiongea na waalimu pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ugala (hawapo pichani) wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa madarasa pamoja na maabara ya Shule ya Sekondari ya Ugala River, iliyopo katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi

Kim Pulsen ataja jeshi la U23
Zuchu kufanya tamasha kubwa Zanzibar watakuwepo hawa