Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Oly Illunga, amejiuzulu kwenye nafasi yake ya Uwaziri, ambapo ameeleza sababu ya kufanya hivyo ni kutoridhishwa na namna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, unavyoshughulikiwa nchini humo.

Akitangaza kujiuzulu kwake, Ilunga amemshutumu Rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi kwa kumteua mtu mwingine kuongoza kikosi kinachokabiliana na ugonjwa huo, ambapo kupitia barua yake ya kujiuzulu Illunga amesema nchi hiyo haina nia thabiti ya kupambana na Ebola.

“Kwa sababu ya uamuzi wa Rais Tshisekedi kuweka mikakati dhidi ya virusi vya Ebola chini ya usimamizi wake moja kwa moja, nimejuzulu kama Waziri wa Afya, ilikuwa heshima kuweka utaalamu wangu na kuihudumia nchi yangu katika miaka hii miwili ya historia yetu,” ameandika kwenye baria yake

Mapema jana Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilitangaza kuwa kutokana na muingiliano mkubwa wa kibiashara kati ya nchi wanachama wa EAC na DR CONGO, upo uwezekano mkubwa wa ugonjwa wa Ebola kusambaa zaidi kutokana mwingiliano wa watu kuzihasa Serikali za EAC kuwa makini na ugonjwa huo.

Dkt. Bashiru aonya ndani ya CCM, 'Wakupuuza tu'
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 24, 2019