Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern amemshusha cheo waziri wa Afya, David Clark kwa kukiuka taratibu zilizowekwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo na kuipeleka familia yake baharini.

Waziri Ardern amesema katika mazingira ya kawaida angemfukuza kabisa kazi Clark kwasababu kitendo alichofanya sio sawa na alitarajia atakuwa mfano kwa wengine.

Aliyekuwa waziri wa afya nchni humo Clark kwa sasa atakuwa katika nafasi za chini za baraza, Katika taarifa yake, amesema hakutumia busara na anaelewa kwanini watu wamekasirishwa.

Hata hivyo New Zealand yenye watu Milioni 5 ilitangaza karantini ya nchi nzima mwishoni mwa mwezi uliopita na kufunga mipaka yake, shule, migahawa pamoja na sehemu nyingine zenye mikusanyiko ya watu.

Ikumbukwe kuwa Idadi ya maambukizi iliyoripotiwa nchini humo ni 1,160 na mpaka sasa kifo kimoja cha mgonjwa wa Corona kimerekodiwa.

Maradona awashauri mastaa wa soka
Corona Ghana: Madaktari kuongezwa mishahara, wananchi kulipiwa bili za maji