Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amethibitika kuonesha dalili za maambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri Mazrui ameonesha dalili za wazi ikiwemo homa kali na maumivu ya viungo huku Akilazimika kupumzika nyumbani kwa kipindi anachougua

Tarehe 22 Disemba 2021 Waziri Mazrui alizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mnazi mmoja akiwataka wananchi kuchukua Tahadhari na wimbi jipya la Corona.

Wito umetolewa kwa wananchi kupata chanjo ili kujikinga na janga la corona.

Zuchu Kinara YouTube
Askofu Desmond Tutu afariki Dunia