Kesi ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi ionayomkaribili aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bernard Murunya imemhusisha aliyekuwa Waziri wa  Maliasili na Utalii wa Serikali ya awamu ya nne, Ezekiel Maige.

Maige alitajwa mahakamani jana na shahidi wa kwanza wa kesi hiyo, Zerari Semfukwe, ambaye ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa Mamlaka hiyo. Aliieleza Mahakama ya Wilaya ya Arusha kuwa Murunya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mamlaka hiyo, Shad Kiambile, waliidhinisha malipo ya dola 66,890, ambazo zilitumika kwa ajili ya safari ya Waziri huyo wa zamani na msaidizi wake pamoja na Murunya mwenyewe.

Shahidi huyo alidai kuwa Murunya na Kiambile ndio walioidhinisha madokezo kwa ajili ya malipo kwa ajili ya safari hiyo.

Semfukwe akiongozwa na wakili wa Serikali, Hamidu Sembano aliiambia mahakama hiyo kuwa utaratibu wa maombi ya safari unatokana na maelekezo ya mkuu wa idara na kujaza fomu inayoonesha anakwenda wapi kwa muda gani.

Hata hivyo, kesi hiyo iliyosikilizwa na Hakimu  Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Arusha, Patricia Kisinda iliahirishwa baada ya kutokea mvutano wa tafsiri za kisheria kati ya Mawakili wa Serikali na upande wa washitakiwa hususan katika kufahamu ni vielelezo vya aina gani ambavyo upande wa mashtaka ulipaswa kuviwasilisha mahakamani hapo.

‘CUF wanajiandaa Kushtukiza Uchaguzi wa Marudio Zanzibar’
Kikwete kuwatumbua majipu wasaliti wa CCM hivi punde