Waziri wa ujenzi uchukuzi  na mwasiliano profesa Makame Mbarawa Leo amezindua  safari za train ya kutoka Dar es salaam  kwenda  Pugu ilikukabiriana na  tatizo la usafiri jijini.
Akizungumza  katika  uzinduzi huo Mbarawa amesema  kuwa train hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba
nakusafrisha abiria  1500 kwa awamu moja,na  itakuwa na safari 3 kwa siku, na kuongeza kuwa train hiyo itakuwa inasafirisha watu 9000 kwa siku.
Aidha aliongeza kuwa serikali inafanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuanzisha usafiri wa boat kutoka posta hadi kijichi kwa ajili ya wakazi wa maeneo hayo.
Hatahivyo  amewataka wananchi wote waliojenga  maeneo ya hifadhi ya reli  kunodoka mara moja kabla hawajachukuliwa hatua za  kisheria na kuwataka pia wafanyakazi wote  wanaofanya kazi kwa mazoea kuacha tabia  hiyo   kwa kuwa serikali ya awamu ya tano haita mvumilia mfanyakazi mzembe.
Tasaf Kunufaisha Kaya Masikini Ilala
Naibu Waziri Mpina Amuwakilisha Makamu Wa Rais Katika Siku Ya KiziMkazi