Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi amemfuta kazi Waziri wa Ulinzi Jaime Augusto Neto, hatua hii inakuja siku moja tu baada ya Rais kumfukuza kazi waziri wa mambo ya ndani, Amade Miquidade.

Pichani ni waziri wa ulinzi Jaime Augusto aliyefutwa kazi na Rais Nyusi

Aidha Rais hajaeleza ni kwanini amewafuta kazi viongozi wakuu wa ulinzi na usalama wa nchi hiyo.

Hata hivyo inaaminika kuwa uamuzi huo unahusiana na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara, mauaji, ugaidi na ufisadi, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya ajali za barabarani, huku baadhi ya kesi hizo zimehusisha askari wa ulinzi na usalama.

Waangalizi wa mambo wamemtaka Rais Nyusi kueleza maamuzi yake ili kuepuka uvumi, hofu na fujo. Wanasema si jambo la kawaida kuwatimua viongozi wawili wakuu wa usalama kwa siku chache na kwamba lazima kuwe na sababu.

Rais wa zamani wa A.K afariki dunia
Haya ndo maajabu ya madaktari bingwa wazawa