Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo, Jim Mattis atastaafu mwishoni mwa mwezi Februari mwakani. Mattis amekuwa akichukuliwa kama mhimili wa utulivu katika baraza la Trump linalobadilika mara kwa mara.

Uamuzi huo wa Mattis ulitarajiwa baada ya tangazo la Rais Trump la kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Syria, hatua ambayo imewakasirisha washauri wake na washirika wa Marekani.

Aidha, katika barua yake ya kujiuzulu, Jim Mattis amesema kuwa anaamini kwa dhati kwamba Marekani inahitaji kuendeleza ushirikiano imara na washirika wake, na kwamba inapaswa kuweka msimamo usio na utata dhidi ya mataifa kama China na Urusi.

Ameweka wazi kwamba, mtazamo wake unatofautiana na ule wa Rais Donald Trump, na hivyo kuondoka kwake kunatoa fursa ya kuteuliwa waziri mpya wa ulinzi ambaye ana maoni sawa na rais.

Hata hivyo, Jenerali huyo mstaafu amesisitiza umuhimu wa kuzingatia mpangilio wa namna dunia inavyoongozwa, ambapo amesema kuwa unasimamia vyema maslahi ya Marekani kiusalama, kiuchumi na kimaadili.

LIVE: Rais Magufuli akiwatunukia vyeo waliofanya vizuri zaidi mafunzo ya uofisa na ukaguzi
Video: Makonda anusurika mtego wa JPM ''Makonda bahati yako sana,''

Comments

comments