Mkuu wa utumishi wa Umma nchini Kenya, Joseph Kinyua ametangaza kifo cha Waziri wa usalama nchini humo Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery  ambaye amefariki dunia saa chache baada ya kulazwa katika hospitali binafsi ya Karen huku akifanyiwa uchunguzi wa matibabu.

“Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,” Amesema Joseph Kinyua.

Kufuatiwa kifo hiko, Waziri Mkuu wa zamani Tanzania, Edward Lowassa ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa usalama wa Kenya.

“Natuma salamu zangu za pole kwa familia na watu wa Kenya kwa kumpoteza Waziri Joseph Nkaissery, alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri wa kupigiwa mfano, Mungu amlaze mahali pema peponi” amesema Lowassa.

Joseph Kasaine Ole Nkaissery alikuwa ni mwanasiasa wa Kenya, Mbunge kutoka mwaka 2002 mpaka 2014 na baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama wa Kenya mpaka kifo chake, mbali na hilo Nkaissery alikuwa kiongozi Mkuu wa jamii ya Maasai nchini Kenya.

 

Fred Matiang'i ateuliwa kukaimu kiti cha waziri usalama Joseph Nkaissery
Bodi ya mikopo kunoa sifa za waombaji, yaandaa vigezo upya