Mbunge wa zamani wa Maswa ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Maji kwa vipindi tofauti, Dkt. Pius Ng’wandu amefariki dunia.

Dk. Ng’wandu amefariki dunia leo katika hospitali ya Somanda, Bariadi alipopelekwa kwa matatizo ya shinikizo la damu.

Waziri huyo amefariki dunia ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu alipofunga ndoa na mkewe.

Aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Maji, Nyumba na Maendeleo ya Mji mwaka 1985 hadi 1987.

Pia, Dk. Ng’wandu alikuwa Waziri wa Maji 1987 hadi 1990, nafasi ambayo aliishika tena mwaka 1996 hadi 1999.

Buriani Ng’wandu!

Baba Jokate afariki dunia
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 19, 2020