Kama wewe ni mtembeleaji mzuri wa kurasa za mitandao ya kijamii ya wasanii wa lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz, bila shaka umekutana na uhaba mzito wa picha zinazowaonesha wakiwa klabu za usiku. Hii imetokana na marufuku inayowakabili!

Mpishi rasmi wa muziki wa WCB ndani ya Wasafi Records, mtarishaji Laizer amesema kuwa moja kati ya sera za lebo hiyo, zinakataza wasanii pamoja na mtayarishaji huyo kwenda kwenye klabu za usiku kula bata.

“Moja kati ya vitu ambavyo tunakatazwa ni kwenda klabu za usiku, hii hairuhusiwi kabisa,” Laizer aliiambia Twenzetu ya Times Fm. “Nadhani ni kwa sababu ya brand, haitakuwa kitu kizuri kuona brand inazurula tu usiku kwenye klabu na kama unavyojua klabu za usiku zina mambo mengi,” aliongeza.

Hata hivyo alisema kuwa wasanii hao wanaruhusiwa kuingia klabu kama kuna kazi au kuna mwaliko maalum utakaowasilishwa kwenye menejimenti kama mwaliko rasmi.

Endelea kubang tu na ngoma za WCB kwenye klabu ya usiku unayoikubali zaidi, lakini usitegemee kumuona Harmonize, Rich Mavoko, Raymond, Lava Lava hata bosi mwenyewe Chibu Dangote wakila bata karibu na wewe ndani ya klabu hizo bila mualiko maalum.

Bulembo awataka viongozi CCM kuwa wazalendo
Mali watetea ubingwa wao AFCON U-17