Rais wa Liberia, George Weah amemtuza aliyekuwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger katika hafla iliyofanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Monrovia.

Rais Weah amempa tuzo ya heshima na ya hadhi ya juu zaidi inayotolewa nchini Liberia ikiwa ni ishara kubwa ya kumshukuru kocha huyo.

Wenger alikuwa kocha wa kwanza wa Rais George Weah kwenye klabu ya Ulaya baada ya Wenger kumleta Monaco 1988.

Aidha, tuzo hiyo si tuzo kuhusu uhusiano wa Rais na Wenger bali inatambua kile Wenger amechangia katika michezo barani Afrika na kuwapa Waafrika wengi fursa kwa mujibu wa waziri wa habari.

Hata hivyo, Rais Weah amesema kuwa Wenger alimtunza kama mtoto wake wakati alipojiunga na Monaco, huku akisema kuwa ‘Mungu ni mkubwa’, kwani bila Wenger hakuwa na namna ya kufika Ulaya.

Mahakama yatupilia mbali madai ya upinzani Zimbabwe
Wapinzani walia na hujuma Kata ya Mbagala Kuu