Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Bodi na Menejimenti ya Mabenki nchini kuwa kuanzia sasa Taasisi zote za fedha ziweke kipaumbele cha kwanza katika kuwezesha na kuendeleza viwanda hasa viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya NBC, ambapo amesema kuwa kama Taasisi hizo zitafanya hivyo zitaweza kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.

Amesema kuwa mabenki mengi yameendelea kutoza riba kubwa hivyo kupelekea wananchi wa kipato cha chini kushindwa kupata mikopo, hivyo amewataka Wataalamu wa NBC na Sekta za Fedha kwa ujumla kutafuta suluhisho la riba zisizo rafiki kwa walio wengi ili amana pamoja na mikopo iweze kuongezeka.

Hata hivyo, Makamu wa Rais ameiagiza Bodi na Menejimeni ya NBC na Mabenki yote nchini kuzingatia Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha kwani Serikali haitamuonea aibu mtu kwa taasisi yeyote itakayokiuka matakwa ya sheria.

 

Mayanga Ataja Taifa Stars Itakayoivaa Botswana
Nuh Mziwanda azungumzia mpango wa kuacha muziki