Wanachama wa klabu ya leo wataingia darasani kujifunza elimu ya hisa katika uwanja wa TCC Chang’ombe, Temeke mjini Dar es Salaam.

Wanachama hao kutoka matawi mbali mbali ya Simba watapewa elimu ya mfumo mpya wa kumilikik hisa za kampuni ndani ya klabu yao.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Simba, Abeid King maarufu ‘Mswati’ alisema elimu hiyo itasaidia wanachama wa Simba kufanya maamuzi sahihi badala ya kukurupuka na kufanya maamuzi ya kishabiki.

Tayari mkutano mkuu wa Simba ulisharidhia mabadiliko ya mfumo ndani ya klabu hiyo ambayo mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ ametoa ofa ya Sh 20 bilioni ili kununua hisa kwa asilimia 51.

“Ni mkutano mkuu wa kihistoria katika Klabu ya Simba, nawasihi wanachama watumie  nafasi hiyo adhimu katika kupata elimu ili kuchagua mfumo wa kibiashara/wa kisasa kama mfumo ufaao kuiendesha ‘Simba Sports Club’.

“Ni mfumo utakaotutoa huku tulikofeli miaka mingi (mfumo wa kadi) na kuja katika mfumo wa hisa ambao unatoa nafasi kwa wawekezaji kuwekeza pesa zao ndani ya klabu yetu pendwa ya Simba.

“Ni mfumo wa dunia ya kileo ya michezo, klabu nyingi zenye kuendelea na kufanikiwa zinatumia mfumo huu wa kibiashara,  mfumo unaowezesha timu kuwa na faida ikiwemo kujiendesha pasipo kumtegemea mtu, kuwa na miundombinu yake kama uwanja, maduka ya jezi, usimamizi mzuri wa masuala ya fedha na wawekezaji kupata gawio lao baada ya faida kupatikana.”alisisitiza King na kuwataka wanachama wa Simba kujitokeze kwa wingi.

Alexandre Lacazette Atuma Salamu, Apiga Tatu Dhidi Ya Nancy
Agosti 14 Haikua Siku Nzuri Kwa Petr Cech