Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lingependa kutoa ufafanuzi kuwa iwapo Bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu 2015/16 inayoendelea atashinda pia taji katika fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ndiye atayeiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.

Kwa msingi huo, timu ambayo itafungwa katika fainali hizo za Kombe la Shirikisho –ASFC linalodhaminiwa na kituo cha Televisheni cha Azam, ndiyo itakayowakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika msimu wa 2016/17

Fainali za Kombe la Shirikisho zinatarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mchuano uliohusisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara – VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).

Kilichojiri baada ya Afisa Elimu kumtwanga makofi mwalimu mbele ya wanafunzi wake
Simba Yashikwa Pabaya Na Baba Wa Soka Duniani (FIFA)