Miss Tanzania wa mwaka 2006, na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu ametangaza kurudi Chama cha Mapinduzi, CCM baada ya miezi ya hivi karibuni kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitokea CCM.

Wema ametangaza kukitupa Chadema na kurudi CCM akidai kukosa amani katika chama hicho.

“Siwezi kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me… Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani…. #ThereIsNoPlaceLikeHome… Feels good to be Back…” amesema Wema Sepetu

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 2, 2017
Picha: Kilimanjaro Stars yafanya mazoezi Machakos Academy.