Wema Sepetu amependa sifa ‘kedekede’ ambazo mama Diamond Platnumz amemwagia mama wa wajukuu wake, Zari The Boss Lady.

Hatua hiyo ya Wema ambaye penzi lake na Diamond liliweka historia ya kuwa gumzo kwenye kiwanda cha burudani nchini imekuja baada ya Bi. Sandra kupost picha ya Zari kwenye mtandao wa Instagram na kumsifu kuwa ni mwanamke msafi, akinukuu mistari ya wimbo wa ‘Iyena’ ambao mrembo huyo kutoka Uganda ameng’arisha video yake.

“Mama Latiffah mwenye … #IYENA yake Mwanamke usafi gaga kulisugua Mume akirudi sharti viatu kumvua… @diamondplatnumz ft @rayvanny.”

Wema na Esma walikuwa miongoni mwa waliopenda (Like) picha hiyo na ujumbe huo.

Hata hivyo, baada ya Wema kuipenda picha hiyo, Esma ambaye ni dada yake Diamond aligawanya sifa nyingine kwa Wema hali iliyomvuta naye kusema yake ya moyoni. Kama ulikuwa hujui, Esma amekujuza kuwa kwenye familia ya Diamond Wema ndiye mbabe wa mapishi.

“Hee kwenye USAFI SASA mama TEE NAMPONGEZA wallah dada msafi huyu kwenye mapishi @wemasepetu unanikomeshaga,” aliandika Esma.

Wema alimjibu wifi yake wanaeitana ‘wifi daima’ (Forever Wiii), “Yaani basi hapo ushamiss mahanjumati… Ngoja nirudi nije nikupikie kipenzi changu…”

Hata hivyo, mitandoa ya kijamii imeibuka na hisia nyingi za sifa hizi na jinsi familia na marafiki wa Diamond walivyoibuka kudai wanammisi Zari baada ya kuachia video ya Iyena inayoonesha tukio la ndoa. Wengi wakitamani ingekuwa ndoa kweli!

Kwa mtazamo mwingine, ni kama imekoreza mkanganyiko wa mahusiano kati ya familia ya Diamond na mpenzi wa sasa, mama mtoto wake pia, mrembo Hamisa Mobeto ambaye anadaiwa kukutana na ‘kipondo’ kutoka kwa Tyyyson Bi. Sandra huko ikulu ndogo ya Madale.

Serikali sasa kutoa ajira ya moja kwa moja kwa wahitimu
Cristiano amuaga Zidane kwa hisia