Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu leo ameita vyombo vya habari na kuzungumza juu ya skendo yake iliyohusisha kuvuja kwa video yake katika mitandao akiwa faragha na aliyemtaja kuwa ni mume wake mtarajiwa.

Wema ameomba radhi, na hizi ndiyo kauli zake alizozitoa hadharani akiwa amemulikwa na vyombo mbalimbali vya habari.

”Ninaomba radhi kwa Serikali yangu kupitia TCRA, nitakuwa binadamu wa ajabu sana iwapo nitasema sijaguswa, nimejikuta kwa mara ya kwanza nimejali tangu jana mpaka sasa siko sawa. Ni kweli nimeudhi wengi, nimekosea na siwezi kumlaumu yeyote”.

”Siombi radhi kwa kutafuta huruma ya mtu yeyote, ila kwa kugundua baya nililolifanya na kukiri ni baya, huenda ni vitendo vya kawaida vinavyofanywa na wote lakini vinapotoka nje huwa vinaleta taswira tofauti  na isiyopendeza na sio kitendo cha kufurahisha kwa namna yeyote ile  na ni zaidi ya aibu na kinapaswa kilaaniwe vikali na nimekosea  na ninaomba  radhi sana kwa waliokwazika kwa upuuzi nilioufanya, mimi ni binadamu tu wa kawaida kama wengine na sina ukamilifu ila muungwana ni yule anayegundua alichokifanya na akakiri”.

”Mimi siyo yule yule wa siku zote, naweze nisieleweke na watu wengi kutokana na historia niliyokuwa nayo, hili limeniamsha, nimeumizwa sana, naomba radhi ndugu zangu, jamaa na marafiki, mama yangu mzazi ambaye alikuwa anaumia zaidi, hakuna marefu yasiyo na ncha, nimefunga jalada la utoto, nimefunga jalada la ujinga, naomba radhi kwa haya yaliyotokea”.

Aidha kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii wa filamu na mzuiki kuvujisha video zao wakiwa faragha hali ambayo inahatarisha maadili ya nchi yetu kwani ni kinyume na maadili yetu.

Mfumo wa kutumia benki za Kiislamu waongezeka barani Afrika
NATO yaanza kufanya mazoezi makali ya kijeshi

Comments

comments