Baada ya Wema Sepetu kupost picha katika mtandao wake wa instagram akiwahimiza watu kumpigia kura Diamond Platnumz katika tuzo za BET na kuibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, malkia huyo wa filamu amefunguka mambo mengi.

Mei 28 mwaka huu Wema alipost picha instagram na kuwataka watu kuwa wazalendo kwa kumpigia kura Diamond Platnumz katika tuzo za BET, lakini picha hiyo iliibua tetesi ya kwamba wawili ambao walikuwa wapenzi kipindi cha nyuma wanataka kurudiana huku mashabiki wengine wakiona kama muigizaji huyo anajitendekeza mbele ya staa huyo wa muziki.

wemake

Mlimbwende huyo wa bongo  amekanusha madai hayo kupitia global online TV,  swala la kutaka kurudiana na Diamond huku akimtakia msanii huyo maisha mema na mpenzi wake wa sasa aitwae Zari.

“Mimi nataka waishi maisha mazuri yeye na mpenzi wake vizuri kwa raha na starehe, kwa sababu simwangalii tena Nasib kama mpenzi, alikuwa, namwangalia kama icon ya muziki, namwangalia kama mwanamuziki mzuri sana” Alisema Wema

Pia Wemaameweka wazi  anatamani siku moja apatane na Diamond na waweze kuzungumza kama washkaji na kufanya biashara kwa pamoja.

DIAMONDWEMA1

“Na nnatamani, one day tuweze hata tuka kaa hivi tukaongea nikamwambia bwana embu tuondokane na mambo haya yote whatever it is me nitakusupport, wewe ukinisupport wala usiponisupport sababu yule naye mswahili sana”

Hata hivyo, Wema amedai Diamond anampinga kwenye mambo yake mengi, na kutolea mfano jinsi Diamond alivyotaka kumpokonya ukumbi wa King Solomon.

“Me naandaa hii show ya Christian Bella, nimepata ukumbi pale King Solomon sawa, yule mtu wa King solomon nimefika pale, tumeshaongea bei ya ukumbi na kila kitu nikamwambia mimi hapa nitakuja kulipa jumatatu, tumeongea ilikuwa Ijumaa, Jumamosi naongea na yule mtu wa King Solomon, Jumatatu naenda pale naambiwa hivi, naambiwa kwamba Diamond anataka kuuchukua ukumbi kwa tarehe hiyohiyo tisa unaona, nikamwambia hivi, nikamwambia hivi ye anataka ku’host party? akanambia nimemwambia ukumbi umechukuliwa akaniuliza na nani, nikamwambia kachukua Wema, akaniambia me niko tayari kupanda dau, Unaona” Wema aliendelea kuelezea “Mwisho wa siku me namchukulia Diamond kama mtu ambaye amekuwa kimuziki lakini yeye ki’personality bado”

 

Zamu ya Akon kutwaa tuzo ya heshima BET baada ya Millen Magese
Bemba ahukumiwa miaka 18 jela