Wema Sepetu aliyekutwa na hatia ya makosa mawili, kutumia pisi tatu za bangi na kukutwa na bangi nyumbani kwake ameamua kulipa faini ya shilingi milioni mbili kama namna ya kuwajibika mara baada ya kukutwa na hatia mahakamani.

Ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimtaka mlimbwende huyo kutoa kiasi hiko cha pesa au kutumikia kifungo jela cha mwaka mmoja.

Taarifa hiyo imetolewa na Wakili wa Wema, Albert Msando ambaye amesema Wema hatotumikia kifungo hicho kwani tayari wameshafanya taratibu za kulipa faini ya milioni mbili kama mahakama ilivyoamuru.

”Kesi hiyo imemalizika leo na hukumu kusomwa ambapo kulikuwa na washtakiwa watatu, mshtakiwa wa pili na watatu wamekutwa hawana hatia na mahakama imewaachia huru na mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Wema Isaack Sepetu amekutwa na hatia kwa makosa yote mawili aliyokuwa anashitakiwa nayo, na mahakama imetoa adhabu ya kulipa milioni moja kwa kila kosa alilokuwa anashitakiwa nalo na akishindwa kulipa anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela, lakini mteja wangu amelipa faini ya milioni mbili hivyo hatatumikia kifungo cha jela kama ambavyo mahakama imeamuru” amesema Wakili Msando.

Aidha Msando amewataka wasanii kutojihusisha na madawa ya kulevya huku akisema kwamba Wema atakuwa balozi mzuri wa kuhimiza vijana na wasanii wenzake kuachana au kutokujiingiza kwenye  matumizi ya dawa za kulevya.

 

Arsene Wenger kukabidhiwa kikosi cha Japan?
Aliyeshinda umiss gerezani ahukumiwa kifo