Menu
 • MARIAM-ID

 • Wema Sepetu apewa ruksa nyingine kwenye Filamu ”Sihitaji kurudi nilipotoka”

  3 months ago Comments Off on Wema Sepetu apewa ruksa nyingine kwenye Filamu ”Sihitaji kurudi nilipotoka”

  Bodi ya filamu nchini imetangaza leo kumfungulia muigizaji Wema Sepetu baada ya kutumikia adhabu yake kwa muda wa miezi minne kutokana na kuvujisha video yake yenye maudhui ya ngono na kusambaa katika mitandao ya kijamii.

  Wema amesema amejifunza na hahitaji kurudi alikotoka ameshaumizwa sana na tabia zake ameahidi kubadilisha mwenendo wake.

  Hivyo Bodi ya Filamu imetoa uamuzi mbele ya vyombo vya habari kupitia kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB),  Joyce Fissoo, ambaye emesema  imeamua kumfungulia Wema  kwa sababu amefuata maelekezo aliyopewa na bodi hiyo kwa asilimia 75.

  “Hatujamfungulia sababu ya huruma, tumemfungulia sababu amefanya tuliyoagiza kwa zaidi ya asilimia 75”, amesema Fissoo.

  Oktoba 26, 2018 Bodi ya Filamu nchini, ilimfungia muigizaji maarufu wa filamu Wema Sepetu kutojishughulisha na uigizaji kwa muda usiojulikana kufuatia picha zake zenye mzudhui yz ngono zilizosambaa mtandaoni Kabla ya kufungiwa.

  Aidha Wakati yote yakijiri mwanadada huyo anatuhumiwa kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wake wa kijamiii ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 21, 2019 kumsomea maelezo ya awali.

  Bilioni 27.4 zapitishwa bajeti ya 2019-2020 Njombe
  Wafanyabiashara soko kuu Mafinga wakarabati barabara za ndani ya soko kuondoa vumbi

  Comments

  comments

  %d bloggers like this: