Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imeamuru aliyekuwa Miss Tanzania 2006 na msanii wa filamu za Bongo, Wema Isaack Sepetu kukaa mahabusu hadi juni 24, 2019 akisubiri uamuzi wa dhamana baada ya kukiuka masharti.

Juni 11, 2019 Mahakama ilimuamuru Wema akamatwe baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa mara nyingine tena huku wakili wake, Ruben Simwanza akieleza kuwa aliuugua ghafla.

Pia, mnamo  mei 14. 2019 Wema Sepetu alishindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kuhudhuria kesi inayomkabili ya kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo wakili wake alieleza mshtakiwa huyo ni mgonjwa.

Aidha kesi yake inatarajiwa kusomwa tena Julai 4, 2019.

Wema Sepetu anashtakiwa kwa kosa la kusambaza picha za ngono kwenye mitandao ya kijamii.

Kosa hilo alilitenda mnamo Oktoba 5, 2018 ambapo picha hizo alizisambaza kupitia mtandao wake wa instagram.

Alikiba afanya mazungumzo na balozi wa Ufaransa
Mwigulu Style inatosha kuwa vazi la taifa- Dkt. Nchemba

Comments

comments