Muigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu, amesema kuna muda anatamani Mungu amchukue afe ili aweze kupumzika na mambo ya dunia ambayo yanamnyima raha.

Wema Sepetu ameyasema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram, akisema ingawa anajua ipo siku atakufa, lakini anatamani ingetokea sasa ili aweze kupumzika na mambo yanayomuumiza nafsi yake ikiwemo kutakanwa bila sababu za msingi kwenye mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu amendeelea kusema kuwa kutokana na mambo ambayo anayapitia anatamani hata asingetokea duniani, na kuamua kukaa nje ya mitandao ya kijamii kwa muda.

“Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele… Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa, “Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema…” Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu… Ya Duniya ni mengi sana”, ameandika Wema Sepetu.

Wema ameendelea kuadniak akisema..” Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist… Ila acha niendelee kumtegemea yeye… Kila jambo hutokea kwa sababu…. Hili nalo litapita… I think I need a Time Off Social Media… Kwa mara nyingine Tena…. Siwezi jamani”.

Licha ya hayo Wema Sepetu hajaweka wazi moja kwa moja ni jambo gani ambalo limemkwaza zaidi, kwani kitendo cha kutukanwa na kusemwa vibaya kwake sio jambo geni.

Ujerumani yatoa fedha kuwasaidia wakimbizi waishio Tanzania na Rwanda
Waziri mkuu Majaliwa akamata Semi Trela 44 Bandarini

Comments

comments