Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imesema haitosita kumfutia dhamana msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu(30), endapo atakiuka tena masharti ya dhamana yake.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu, Juni 24, 2019 na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana.

“Mahakama inatoa onyo la mwisho kwa mshtakiwa, ikitokea mshtakiwa huyu amevunja sheria kwa kutokufika mahakamani bila taarifa, Mahakama hii haitasita kumfutia dhamana.”

Hivyo mahakama imemrudishia dhamana Wema Sepetu na kumruhusu aendelee na kifungo chake cha nje mara baada ya kutumikia kifungo cha ndani Segerea kwa muda wa siku 7 tangu aliposhikiliwa.

Mahakama ya Kisutu, ilitoa hati ya kumkamata Wema, Juni 11, 2019 na mshtakiwa huyo kuruka dhamana na kujisalimisha Juni 17, 2019  baada ya Mahakama kutoa hati ya kumkamata Wema Sepetu kutokana na kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa.

Ambapo Mahakama iliamuru msanii huyo anakabiliwa na kosa la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandaoni wa Istagramu kinyume cha sheria kuwekwa rumande hadi leo Jumatatu.

Hakimu Maira ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 itakapoanza kusikilizwa ushahidi.

Askari 6 mbaroni kwa kuomba rushwa ya milioni 8 kwa mzee wa miaka 95
Je unatafuta ajira?, Hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako