Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu, maarufu kama Madam Wema amefunguka rasmi kuwa hivi karibuni Diamond Platinumz ambaye amewahi kuwa nae kimahusiano atakuwa bosi wake kupitia chaneli yake mpya inayofunguliwa ya Wasafi TV.

Wema Sepetu amesema kupitia Wasafi TV, atakuwa anaendesha kipindi chake hivyo Diamond atakuwa bosi wake.

”Na Diamond anaenda kuwa bosi wangu nitakuwa na kipindi Wasafi TV” amesema Wema.

Wema amefunguka hayo alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu sakata la Diamond na Zari kuachana, ambapo kwa mujibu wa Zari Hassan alipohojiwa BBC Swahili alitaja moja ya chanzo cha kuvunja mahusiano yake na Diamond ni video za Daimond na Wema zilizosambaa mtandaoni zikiwaonesha wawili hao kuwa karibu sana.

Wema amekanusha tuhuma zinazodai kuwa yeye ndio chanzo cha wawili hao kuachana na amesema kuwa inawezekana Zari ameamua kumuacha Diamond kwa vitu vingine vya nyuma, kwani yeye na Diamond siku ile hawakukisiana kama ambavyo wengi wanasema kikubwa tu walikumbatiana kama marafiki.

”Kumkumbatia au yeye kunikumbatia haimaniishi kuwa mimi na yeye ni wapenzi mimi na Diamond ni marafiki wazuri” amesema Wema

Aidha ameongezea kuwa yeye na Diamond wameamua kukua ndio maana wameamua kuweka tofauti zao pembeni na kupeana sapoti katika kazi.

Pia ameongezea kuwa yeye hawezi kuwa mshauri wa Zari, kikubwa tu Zari akae na mwanaume wake wayamalize, amethibitisha tu yeye kwa sasa hana mapenzi yeyote na Diamond.

Hali ya Mbowe kiafya yatetema, akimbizwa KCMC
Nape: Huu ni ushetani wa baadhi ya viongozi wa Afrika

Comments

comments