Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger sasa anaamini kwamba kikosi chake kipo tayari kushinda taji la ligi kuu soka Uingereza msimu ujao.

Bosi huyo wa Gunners anajiamini kwamba timu yake itawazuia Chelsea kutetea ubingwa wao, huku akikanusha kuwa Arsenal ni dhaifu mbele ya  The Blues.

Arsenal haijawahi kushinda kombe tangu 2004, mwaka ambao Jose Mourinho aliwasili jijini London, lakini Wenger ambaye hajawahi kumfunga Mourinho amewaambia waandishi wa habari:

“Tutashinda ubingwa msimu ujao? huwezi kujipa uhakika katika michuano ya ligi kuu. Nataka kusema kwamba, tutapambana kuwania ubingwa. Nikiwa kocha lazima niisaidie timu, lakini mwisho wa siku najua mwishoni mwa msimu nitakuwa wapi”.

Kuanzia Agosti 8 mwaka huu, Arsenal wataungana na Manchester City, Manchester United kuwania ubingwa ambao unashikiliwaa na Chelsea

Wagombea CCM Wapigana Ngumi
Ronaldo Amuwakia Kocha Wake Benitez