Kocha wa Klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa mchezo wa mpira wa miguu barani ulaya unaharibiwa na fedha ambapo zimekuwa zikitumika kwa kiasi kikubwa.

Amesema kuwa kwa sasa hakuna tena utabiri wa timu kuchukua ubingwa kama ilivyokuwa hapo awali kwani kinachotawala ni pesa.

“Unapozitazama ligi tano barani Ulaya mnamo mwezi Disemba, unaweza kujua ni timu gani zitakazoshinda ligi zao kwakuwa zinajionyesha.”amesema Wenger

Aidha, ametolea mfano wa timu kama PSG iko pointi 11 juu katika ligi ya kwanza , Bayern Munich iko pointi 16 juu katika ligi ya Bundesliga na Manchester City ipo pointi 15 juu ya jedwali la ligi ya Uingereza.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa mpangilio huo lazima kuna kitu ambacho hakiko sawa kwenye mchezo huo kwani utajiri mkubwa wa baadhi ya timu unaharibu ushindani uliokuwepo hapo awali.

 

Waziri Jafo awaweka mtegoni Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi
Video: Familia yakuna kichwa mazishi ya Kingunge, Zitto Kabwe 'ajivisha mabomu'