Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, amesema alishangazwa kuona aliyekua mshambuliaji wake Nicklas Bendtner, amejiunga na kikosi cha Nottingham Forest, kinachoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England.

Wenger amezungumzia kushangazwa na uhamisho wa mshambuliaji huyo ambaye alionyesha utovu wa nidhamu wakati akiwa Emirates Stadium, huku kikosi cha The Gunners kikitarajia kupambana na Nottingham Forest katika mchezo wa kombe la ligi (EFL) ambao utachezwa hii leo huko City Ground.

“Ilinishangaza kuona Nicklas amesaini kuitumikia Nottingham Forest, lakini wakati mwingine niliamini huenda anatafua mahala pa kuanzia ili afikie lengo la kucheza katika kiwango cha juu kama ilivyokua,” Wenger amenukuliwa na tofuti ya Arsenal (www.arsenal.com)

“Wakati mwingine kama unatambua thamani ya uchezaji wako, unapaswa kujipima na kujua unastahili kuanzia wapi ili kiwango ulichokua nacho kirejee, najua anataka kucheza kila mara ndio maana ameamua kwenda huko.

“Ni kweli anahitaji kuthibitisha uwezo wake. Japo aliwahi kuwika akiwa na Arsenal na klabu nyingine kama Birmingham City, Juventus na    VfL Wolfsburg.

Bendtner mwenye umri wa miaka 28, alijiunga na Forest kama mchezaji huru mapema mwezi huu, baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya VfL Wolfsburg inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ujerumani.

Akiwa na klabu ya Arsenal kuanzia mwaka 2005 hadi 2014, mshambuliaji huyo kutoka nchini Denmark, alicheza michezo 108 na kufunga mabao 24, na kati ya michezo hiyo, 83 alianzishwa katika kikosi cha kwanza.

Claudio Ranieri Asisitiza Heshima Kwa N'Golo Kante
Ronaldo, Bale Waongeza Chachu Ya Ushindi Wa 17