Wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto ambayo ilianza Agosti mosi 2022 na imeadhimishwa Duniani kote kwa jamii kuelimishwa kuhusu umuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto ambapo wengi wao wameonekana kuepuka maradhi ya Polio kwa watoto kutokana na kuzingatia suala la unyonyeshaji.

Wiki hiyo ambayo imehitimishwa rasmi Agosti 7, 2022 imetoa kutoa uzoefu juu ya masuala ya unyonyeshaji kwa akina mama, ambapo wachache kati ya hao walikuwa wamekumbwa na kasumba ya kupenda maziwa ya kununua bila kuzingatia ushauri wa kitaalamu kiafya.

Mkoani Morogoro, kwa wiki nzima mashirika mbalimbali kwa kushirikiana na serikali yamekuwa yakizungumza na wanajamii ili kufahamu uelewa wao kuhusu suala hili la unyonyeshaji na pia kuwapa elimu kulingana na eneo linalohitajika.

Mmoja wa wanawake waliohudhuria maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Fadhila Yusufu anasema unyonyeshaji kwake ni kipaumbele kikuu kwa mtoto wake na kusema, “Elimu niliyoipata katika wiki hii itaniongeza juhudi za unyonyeshaji.”

K wa upande wake, mtoa huduma za afya kitengo cha Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kata ya Mkambalani Rebeka Wami, amethibitisha kuwa wanawake wana mwamko wa kunyonyesha watoto wao kwa mujibu wa malekezo ya wataalamu wa afya.

Mtoa huduma za Afya kitengo cha Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kata ya Mkambalani, Rebeca Wami akizungumza na mama aliyehudhuria mafunzo wakati wa wiki ya unyonyeshaji. (picha na Hamad Rashid /UN).

Amesema, “Katika siku yetu hii ya unyonyeshaji, tumeweza kupata uzoefu wa kipekee ambao tumeona akina mama wengi wanahamasika na unyonyeshaji wa maziwa pekee kwa mtoto chini ya miezi sita.”

Ukanda wa Morogoro katika eneo la Mkambarani pekee, akina mama wengi wanaonekana wamepata elimu ambayo imeweza kuwasaidia kunyonyesha watoto wao na kuondoa hali ya utapiamlo huku suala la uzingatiaji masuala ya afya yakipewa kipaumbele.

Bondia Shaban Kaoneka avitupia lawama Vyombo vya Habari
Wakenya waishio Ughaibuni kupiga kura